MIMBA ZA UTOTONI HUTOKEA SANA KIPINDI HIKI
Zamani tatizo la kupata mimba utotoni lilikuwa ni kwa familia za hali ya chini kielimu na kiuchumi, laikini kwa sasa janga hili limekuwa ni kwa wote hadi kufikia hatua ya serikali na taasisi za haki za kibinadamu kuingilia kati.
Jamii nyingi hasa zakiafrika bado zinaumiza kichwa juu ya ufumbuzi wa tatizo hili, chanzo chake na suluhu lake. Baada ya kupitia tafiti nyingi leo nakuletea somo juu ya tatizo hili.
Tafiti nyingi zinasema Mimba za utotoni zinatokea hasa kipindi cha likizo
Kipindi cha likizo au kipindi ambacho watoto watoto wa shule wapo nyumbani kwa mapumziko, ni kipindi hatari hasa kwa mtoto wa kike. Na kwa kipindi kama hiki ambacho watoto wapo nyumbani, ni kipindi ambacho mzazi na jamii nzima inatakiwa kuwa makini juu ya mtoto wa kike ili kuhakikisha anatimiza ndoto zake.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo kuhusu kipindi cha likizo.
- Kipindi cha likizo, ni kipindi ambacho kwa asilimia kubwa mwili wa mwanafunzi unafanya kazi nyingi (physical work), na kupelekea mzunguko wa damu katika mwili kuwa mzuri Zaidi na kupelekea baadhi ya vichochezi vya mwili (hormones) kusafirishwa kwa kasi sana.
- Kipindi cha likizo ni kipindi ambacho ubongo wa mwanafunzi hupunguza umakini katika mambo ya shule na kuweka umakini Zaidi katika mambo ya maisha bila kujali hatari wala faida.
- Kipindi cha likizo ni kipindi ambacho akili ya mwanafunzi, (awe wa kiume au wa kike) hukutana na watu wapya, vivutio na vishawishi vingi vipya, hivyo kupelekea kushindwa kuvumilia.
- Kipindi cha likizo ni kipindi ambacho mambo mengi hutokea. Siwezi taja yote, bali tuone ni jinsi gani tunaweza wasaidia waoto wetu kuepukana na janga hili la mimba za utotoni linalopelekea kusitisha ndoto zao.
Kutokana na baadhi ya hatari ambazo zinaweza pelekea kukatisha ndoto za mtoto wa kike, kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza kufanya wewe kama mzazi au mlezi ili kuokoa ndoto zake.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo unaweza kufanya wewe kama mzazi au mlezi kwa mwanafunzi ili kuepusha mimba za utotoni.
- Kuwa na desturi ya kuongea na mtoto hasa mazungumzo ya maisha, mambo ambayo anaweza kufanya ili kufikia ndoto zake, na mambo ambayo yanawezapelekea kukatisha ndoto zake.
- Mshughulishe mtoto hasa katika mambo ya masomo, mpatie pia muda wa kupitia masomo yake
- Epuka kumpa mtoto (hasa wa kike) uhuru wa kwenda mahali usipopajua na kwa muda mrefu.
- Epuka kumwacha mtoto kuwa na mazoea na watu wa jinsia tofauti kwa kiasi cha kupitiliza.
- Usimruhusu mtoto kutoka nyumbani masaa ya joini au usiku bila sababu maalumu nay a msingi.
- Kuwa na tabia ya kufuatilia mienendo ya mwanao, maongezi, uvaaji na mabadiliko ya tabia katika lugha na mawasiliano.
- Epuka kumwacha mwanao bila shughuli ya kufanya kwa siku au wiki nzima, na epuka kumfanyisha mwanao shughuli nyingi hadi kufikia kuchoka. Hii inaweza kumpelekea mwanao kuwa na hisia kali za kimahusiano.
- Hakikisha hauwi mkali wala mpole kwa mwanao kiasi cha kupitiliza. Hii inaweza kumfanya mwanao kuzoea hali yako na kumpelekea kujaribu mambo mapya hasa unayomkaripia au yale usiyoyajali.
- Kuwa na mahusiano mazuri na mwanao hadi kufikia hatua ya mwanao kuwa huru kukwambia jambo lolote hata liwe na usiri wa namna gani. Mzazi unapaswa kuwa rafiki wa kwanza kwa mwanao.
- Epuka kumkaripia mwanao unapomfundisha juu ya maisha.
Hayo ni baadhi ya mambo ya kufanya ili kuzuia mimba za utotoni, ni jukumu langu mimi na wewe kuhakikisha tunamlinda mtoto wa kike, na kuhakikisha anafikia ndoto zake za kielimu.
By. Rodger Adr
Comments
Post a Comment