Chuchumaa
Acha Kukaa Tu!
Kuchuchumaa ni mkao wa asili ambao una faida nyingi kwa afya ya binadamu. Kabla ya uvumbuzi wa viti, makochi na masofa ya kifahari, watu waliishi kwa kupiga magoti, kuchuchumaa, kulala au kusimama mikao hii ilihusisha mwili mzima na kusaidia afya kwa ujumla.
Faida za Kuchuchumaa:
- Huhusisha na kuimarisha misuli yote ya sehemu ya chini ya mwili.
- Husaidia mzunguko mzuri wa damu na kurahisisha kazi ya moyo.
- Husaidia mwili kutumia sukari na mafuta kwa ufanisi hupunguza hatari ya kisukari na mafuta mabaya mwilini.
- Huongeza kasi ya uchakataji wa chakula (metabolism).
- Hupunguza uwezekano wa kupata maumivu ya mgongo, kiuno na matatizo ya mpangilio wa mgongo.
Madhara ya Kukaa Muda Mrefu:
- Kukaa muda mrefu kunachangia magonjwa sugu kama kisukari aina ya pili, matatizo ya moyo, na hata vifo vya mapema.
- Watu wanaokaa muda mrefu, hasa kazini, mara nyingi hupata maumivu ya mgongo na kiuno kutokana na mikao mibaya.
Mfano, kwa jamii kama Wahadzabe, hata wazee wa zaidi ya miaka 60 bado wanachuchumaa kwa urahisi. Lakini mijini hali ni tofauti kwa sababu watu wamezoea maisha ya starehe na kusahau namna ya kuutumia mwili ipasavyo.
Nakushauri;
- Hakikisha unachuchumaa kila siku.
- Punguza muda wa kukaa bila kusimama au kutembea.
- Usisahau mazoezi ya miguu unapoenda mazoezini.
Kumbuka: kukaa kwa starehe kupita kiasi kunaweza kuathiri afya yako. Chuchumaa, tembea fuata njia ya asili ili kuishi kwa afya bora!
✍π½✍π½✍π½✍π½
Comments
Post a Comment