AMUA KUPAMBANA

Safari ya kuitafuta furaha yako binafsi haiwezi kuwa rahisi, 


Kiu ya kufikia malengo yako kamwe sio rahisi, Utapingwa, Utakatishwa tamaa, Utadanganywa, Utakwazwa, Utatapeliwa, Maranyingine watu watakao kukwamisha ni wale walio karibu sana na wewe, Watu uliodhani watakusaidia kufikia lengo lakini unakuta ndio viongozi wa kuhakikisha hupigi hatua, 

Ukiamua kukata tamaa basi utawafurahisha na kamwe hufiki popote,

  Piga moyo konde, amua kupambana na kila kikwazo na usisahau kuwa vikwazo vingine viko ndani yako wewe mwenyewe, vikwazo hivyo ni hatari kuliko vile vilivyo nje yako. Ukiamua utashinda.


AMUA KUPAMBANA

Comments