UGUMBA KWA MWANAMKE

 

UGUMBA KWA MWANAMKE (KUTOSHIKA MIMBA – SABABU NA MATIBABU)

Ugumba

Ugumba ni hali ya kupoteza uwezo wa kushika ujauzito, baada ya mme na mke kukutana kimwili bila kinga kwa mwaka mzima.

 

Kwa mwanamke aliyekatika umri wa kuzaa, anatakiwa apate ujauzito ndani ya mwaka mmoja baada ya kuolewa au kuwa kwenye mahusiano na mme.

Ujauzito unapatikana baada ya mwanamke kukutana na mwanamme kimwili na kwa ukamilifu katika siku za hatari za mwanamke (kipindi cha uchavushaji wa yai la kike). Na katika hili, mwanamme awe na uwezo wa kutoa mbegu za kiume imara wakati wa tendo la ndoa.

 

AINA ZA UGUMBA (Infertility)

1.      Primary infertility (Aina ya kwanza)

Hii hutokea pale mke na mme, tangu waoane au tangu wawe kwenye mahusiano, hawajawahi kupata mtoto licha ya kukutana kimwili na bila kinga yoyote.


2.      Secondary Infertility (Aina ya pili)

 Hii hutokea pale mke na mme ambao waliwahi kupata mtoto, wanakosa uwezo wa kupata/ kuzaa mtoto mwingine licha ya kukutana kimwili mara kwa mara na bila kinga.


Sababu za Ugumba

1. Mvurugiko wa vichochezi vya mwili (Hormonal imbalance)

2. Kuziba kwa mirija ya uzazi

3.      Magonjwa kwenye mfumo wa uzazi (PID)

4.      Uvimbe katika mji wa mimba (Uterine Fibroids)

5.      Msongo wa mawazo (emotional Stress)

6.      Uzito kupita kiasi (Over wheight)

7.      Utoaji wa mimba (Abortion) wa mara kwa mara

8.      Matumizi ya Sigara, Pombe au Vilevi


9.      Mzunguko (Menstrual Period) isiyoeleweka

10.  Umri mkubwa (Zaidi ya miaka 35)

 

Dalili za Ugumba

1.      Maumivu chini ya kitovu

2.      Maumivu ya kiuno na mgongo

3.      Mzunguko usioeleweka au ulioambatana na maumivu

4.      Kukosa hamu ya tendo la ndoa




Tiba ya Ugumba kwa mwanamke

1.      Acha matumizi ya pombe, sigara na vilevi vingine

2.      Epuka visababishi

3.      Tibu magonjwa ya zinaa n.k.

4.      Kutana na mme kipindi hasa kwenye siku za hatari

5.      Dhibiti uzito iwapo umezidi

6.      Fanya mazoezi ya mwili na lishe bora

 


Hayo ni miongoni mwa mambo unayoweza kufanya ili kuepukana na hilo tatizo, ila kama umesumbuka saana na hili tatizo, usisite kuwasiliana nami kwa simu namba 0744925651 kwa ushauri na tiba Zaidi.

Ugumba kwa mwanamke unatibika

Comments

  1. Somo hili ni miongoni mwa masomo yaliyoleta utatuzi wa changamoto kwa wengi.

    ReplyDelete

Post a Comment